Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Sawasawa haya asante hiyo tumemaliza nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18272_001 hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hicho?
R: Kikapu
I: Kikapu?
R: Eeeeh
I: Kikapu kisambaa kinaitwaje?
R: “ngahu”
I: „ngahu“?
R: Eeeeh hahahahhah
I: Hahahahahah „ngahu“ ni watu gani wa utamaduni gani wanatumia „ngahu“?
R: Watu wa Tanga
I: Makabila gani unaweza ukaya taja?
R: Hii kapu haina mdigo, msambaa, mbondei, mzigua
I: Na unaweza kutuambia inatumikaje?
R: Saa nyingine ukienda mashine unaweka mahindi yako na makopa yako unapeleka mashine unaweka kwenye kapu na safari mnaenda wanawake mnapeleka tunaita ushashi kumuangalia mzazi lazima pale kila mama anakuwa kabeba kapu yake
I: Kwanini ilikuwa lazima uwe na kikapu ukienda kuangalia mzazi?
R: Ndiyo utamaduni wetu tuseme eeeh
I: Ni utamaduni?
R: Eeeh
I: Kwahiyo mtu hawezi kubeba hivi hivi bila kikapu?
R: Saivi mtu na begi lake la mgongoni kaweka mfuko wake wa magufuli unga na sabuni hana habari na kikapu
I: Kwa kipindi hicho ilikuwa ina hadhi gani kubeba kikapu kwenda kwa mzazi?
R: Hadhi sasa ukienda pale unapokelewa kapu kama huna kapu unadharaulika sana kwahiyo lazima uwe nalo
I: Kwahiyo ilikuwa unapewa hadhi kubwa ukibeba?
R: Kikapu
I: Na waliokuwa wanabeba Zaidi kikapu ni watu gani?
R: Wasambaa
I: Wa jinsia gani?
R: Wabondei, wazigua, wasambaa wenyewe wa Lushoto
I: Wakike au wakiume?
R: Wa kike
I: Kuanzia umri gani au mtu yoyote tu wa umri wowote anaweza akabeba kikapu?
R: Anabeba
I: Ilikuwa haijalishi umri?
R: Hapana mtu ukienda safarini hivi si mgeni lazima uwe na kikapu chako tena zamani kilikuwa kinawekwa bahasha kabisa ukifika kikapu pale kinafunguliwa basi ndiyo furaha kwamba mgeni kaja
I: Sawasawa na kwa mawazo yako unadhani kikapu kina nafasi kwa hali ya sasa?
R: Ndiyo eeh
I: Unadhani inaweza ikafika kipindi kikawa hakitumiki tena?
R: Kwa hawa wenzetu wanaokuja miaka ijayo sidhani kama kitakuwa na hadhi tena
I: Kwanini?
R: Basi siwanaenda na wakati eeh wana vikapu vyao
I: Vya aina gani?
R: Manila hivi
I: Aaaaaaa vya manila?
R: Eeeh
I: Kwahiyo hivo vinaenda vinapotea?
R: Hivi vinapotea
I: Na ili uweze kutumia kikapu ulikuwa unatakiwa uwe na kitu gani kingine?
R: Ukiwa na kikapu ni muhimu tu ukiwa na kikapu
I: Kikapu tu basi hakuna kitu ambacho lazima uwe nacho ndiyo uwe na kikapu?
R: Kikapu unaweka zile zawadi zako unaziweka kwenye kikapu
I: Kwahiyo kilikuwa kinatumika Zaidi unapoenda kumuona mzazi?
R: Hata ukienda safarini mgeni unaenda lazima unabeba kikapu chako eeh
I: Sawa sawa
R: Unapoenda kumuona mgonjwa unabeba kikapu eeh umeweka vya kuweka humo na zawadi pia
I: Vikapu kama hivo vinatengenezwa katika maisha yetu ya sasa hivi?
R: Wanatengeneza sana wazigua
I: Wazigua?
R: Eeeh
I: Handeni handeni huko?
R: Eeeeh
I: Ndiyo wanatengeneza sana
R: Eeeeh
I: Sawa na wanaotengeneza vikapu ni kina nani hasa ni jinsia gani na waumri gani katika jamii yenu?
R: Siku hizi kwa vile wabunifu ni wengi hata wasichana mtu anasuka vikapu vyake hapo basi anakuja ananunua mtu anakwenda kuuza huko
I: Kwahiyo saivi haijalishi umri?
R: Hapana
I: Wala jinsia?
R: Hapana
I: Labda miaka hiyo kikapu kilikua kinatumika kubebea vitu wakati unaenda kumuona mzazi walikuwa wakitengeneza watu wa jinsia gani kwa kipindi hicho na umri wao ulikuwa je hao waliokuwa wanatengeneza?
R: Walikuwa ni wababa tu
I: Kuanzia umri gani?
R: Kuanzia miaka thelathini kwenda juu
I: Kwenda juu?
R: Eeeeh
I: Unaweza ukafahamu ni nyenzo gani zinatumika kutengenezea kikapu?
R: Kuna minyaa
I: Minyaa ndiyo nini?
R: Ule ukindu
I: Ukindu?
R: Eeeh kuna ule mwingine ule sijui wanaitaje
I: Ukindu au minyaa?
R: Ukindu sijui wanaita minyaa na kuna wengine wanasema mfuko wa mabamba
I: Mfuko wa mabamba?
R: Eeeeh ndiyo hiyo minyaa sijui
I: Ni kitu gani kingine ni hiyo minyaa tu na ukindu basi?
R: Eeeh hiyo tu
I: Ndiyo hizo zilikuwa zikitumika kutengeneza kipindi hicho na sasa hivi zilikuwa zikibadilika au hazibadiliki?
R: Eeeeh wanabadilisha
I: Labda kwasasa?
R: Vikapu unashika huku na huku vile vya ukindu labda nikuonyeshe fashion yake
I: Utanionesha sawa bado ukindu unaendelea kutumika kutengenezea hivo ama?
R: Ndiyo
I: Hakuna material nyingine zinatumika?
R: Vikapu wanatengenezea ukindu na makawa eeh
I: Sawasawa
R: Hiyo ipo kama ilivo
I: Sawasawa nitapiga picha hizo sawa na kwa hicho jinsi unavokiona kikiletwa saivi kwenye masoko yetu ya kisasa kinaweza kikauzwa shilingi ngapi?
R: Kuanzia elfu tano na kupanda juu
I: Kuanzia elfu tano na kupanda juu kwasababu gani kinaweza kikauzwa elfu tano na kupanda juu?
R: Saivi vina gharama yake saivi vinapatikana tuseme kwa shida
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 6
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali