Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Kisu chenye mshikio wa mbao

Sammlung Braun
r 2018 / 18232
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18232
Kichwa
Kisu chenye mshikio wa mbao
Vipimo
Urefu: 13cm
Nyenzo
Wood,
Chuma
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_03279567-1d1f-47b5-92c9-46753c0cfc01
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1920
Mtu
  • Person (Mtengenezaji)
Mahali
  • Tansania
Acquisition:
Wakati
ca. 1904 - ca. 1920
Mtu
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Sawasawa asante nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18232_1 kuna mtu aliitambua hii inaitwaje kimasai hii? R2: Engalemu maana hiyo sahivi hii iko ndani ya mila mpaka sahivi mzee akitoka kuchinja dume lale au chochote tu ni kisu ambacho kipo vizuri anahalalisha hakifanyii kitu chochote ni kuchinjia dume la ng’ombe maana hiyo inaitwa engaremu I: Kwahiyo ni kwa ajili ya kuchinja tu dume la ng’ombe au kuna matumizi mengine kinatumika namba mbili hebu tuambie? R2: Eeeeh I: Na anayekaa nacho hicho kisu ni nani? R2: Mzee I: Wakuanzia umri gani? R2: Mzee ndiyo anaweka sehemu yake au unamkuta mke wako uliye muamini sema haendi kutumia kwenye matumizi mengine anapewa anaweka kama hii maana haiwezi kuguswa na mtu mwingine I: Haiguswi na mtu mwingine? R2: Eeeeeh I: Na wanaotengeneza hiyo ni kina nani? R2: Wazee R1: Hichi ni kisu najua kinatumika kwa vitu vingi sana moja mzee anaweza akatumia kwa ajili ya kuchinjia mbili kuna kipindi unakuta sasa hivi kama tuseme huyu baba ameshafikia umri wake sasa hivi na sisi ni rika nyingine tukishaelekea kwenye upande wa rika kuna dume ambalo tunachinjaga kulingana na watoto uliopata kumaanisha umekuwa mzee sasa ni kama dume la shukurani kwa jamii wote maana mtu kama huna watoto huwezi ukachinja hilo dume yani ni ile tu kwamba ni shukurani kutoka kwa watu na pia kuonekana na wewe umeshaingia kwenye lile group la watu wa rika kwahiyo ni shukurani unatoa kwa jamii nzima kwa kuchinja dume hilo la ng’ombe I: Ni rika gani hiyo ambayo ukiingia lazima uchinje dume la ng’ombe namba moja tuelezea hapa? R1: Yani inategemea na kundi kutolewa kwahiyo unaweza ukakaa tu ukiwa mtoto mdogo umekuwa kijana umetahiriwa bado huna mwanamke unavokuja umeoa umepata watoto wako sasa ukishaanza kuwa na watoto maana bila watoto huwezi kuchinja ile dume la ng’ombe ila kwa vile umepata watoto umepata mvulana, msichana sasa unaanza kuchinja yani inaonekana kabisa kihalisia lile dume nila shukrani na ukishamaliza ile sasa hapo umeshamaliza mambo ya vijana umekuwa mzee unaelekea kwenye kundi la wazee ushaachana na vijana na shukurani umeshatoa na vitu ulivyopata chini ya ardhi hivyo ndivyo ilivyokuwa inafanyika katika jamii yetu ya kimasai I: Na bado kinatumika mpaka hivi sasa? R1: Eeeeh kisu bado kinatumika sanasana kinakuwa ni kisu kwa ajili ya mzee na kama mzee ana nyumba yake ataenda kuweka kwake na kama ana mwanamke anamwamini anaweza akampa na anaweza akalaani hata isiguswe kabisa ndani ya boma mpaka yeye aruhusu iguswe au aje kuigusa mwenyewe hizi zote ni tamaduni, mila na desturi katika jamii yetu hii ya kimasai na lazima zizingatiwe R3: Matumizi ni kuchinja ng’ombe ile ya rika ni baada ya kuwa mzee kwasababu siumekuwa mtoto ukawa morani, sasa unaonyesha sasa umekuwa mzee na una watoto wako huweki tena sehemu kwahiyo mtu kama amekuwa mzee ndiyo anachinja I: Ndiyo anachinja? R3: Eeeeh inaonyesha sasa kazi imeisha I: Na hii Engalemu ilikuwa inatengenezwa kwa kutumia nini na nini namba tatu hebu tuambie hapo? R3: Inatengenezwa kwa kutumia vijiti unaweka vijiti alafu unaweka hii chuma R2: Unjaua hii hizo ni chuma za kizamani wanaojua hata mfupa ina haribu kabisa hiyo inatengeneza kutafuta hizo kitu inayoitwa tupa kutengeneza kabisa na kutengeneza vizuri na kutafuta hivi vijiti na kuweka vizuri I: Hii njiti iliyokuwa inatumika ni njiti ya namna gani? R2: Hiyo ni aina ya miti ya olitepesi mizizi yake ya ndani I: Kwanini mzizi? R2: Ndiyo ngumu haiwezi kupasuka unaweka olitepesi au osilale hii yote ni miti ambayo haipasuki I: Kwahiyo ilikuwa ina umuhimu mkubwa sana kwenye jamii? R2: Eeeh kwenye mila na desturi I: Kwahiyo ni mzee au mke anayemwamini ndiyo anampa kuhifadhi hicho namba mbili hebu tueleze? R2: Eeeeh kuhifadhi lakini siyo kutumia I: Ni kwa ajili ya matumizi ya kuchinja tu? R2: Kabisa hiyo tu katika boma lako lazima iwe nayo hii kisu I: Kwahiyo kila boma lazima iwe nayo? R2: Eeeh kisu ya mzee

chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 06
mwandishi: I: Mohamed Seif, R1, R2, R3: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Orbomba
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-03-14, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (82)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (8)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1904-11-27, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 43 (103)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:01:51+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji