Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/1

Kijiko cha mbao

Sammlung Braun
r 2018 / 18311
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18311
Kichwa
Kijiko cha mbao
Vipimo
Urefu: 25,7cm
Nyenzo
Mbao
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_47f89faf-4975-4c9e-af6a-62faa63810da
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Utunzaji wa nyumba  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1905-12-24
Mahali
  • Tansania
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Kununua / Uuzaji
Wakati
1905-12-24
Maelezo
"Jumapili 24. Mwezi wa kuminambili 1905. [imepigwa mstari, u. 60] [u. 61] [...] jioni imekwenda [...] [?] yenye thamani ya kimila. Karibu zote nimetafutiwa na Max. Kasha ya ugoro kutoka pembe & ubao imenunuliwa hapa kutoka Mswahili (1 Rup.) Picha cha kufanana. kwa Baumann. Usambara. 1891. u. 231. / kisuaheli: tabakero imetengenezwa na Wanjamwezi [mchoro wenye maelezo ya vilivyotumika] mbao pembe mbao / vitana, 3 kama vile nilivyovichora shajara 44, u .68. Kitana kimoja kama picha hapo & kimoja nimechongewa na Mnyamwezi hivi karibuni jina lake [?] kina umbile kifuatacho [mchoro] / kisuaheli: chanuo / kimetengenezwa kutoka mbao mweupe laini bila kupigwa msasa [u. 62], wakati vingine vinatokana [sic] na fundi hutu huyu mmoja (fundi) anayekuwa fundi maalum kwa kutengeneza vitana. Hivi vina rangi ya manjano na ni laini. [mchoro] / vijiko vidogo na vikubwa zaidi vilivyochongwa vyenye mabambo ya kuchoma vina umbile vya mduara vingine havina kina vingine vyenye kina zaidi mapambo ya kuchora viko tofauti tofauti [michoro ya vijiko saba a-g, mingine yenye umakini upande wa mapambo yenye maelezo] kisuaheli: kijiko / mwiko / wu bu [?] / kijiko chenye kina kirefu: [mchoro h] [mchoro wa fidla wenye maelezo ya mali ghafi] fidla ya mbao shaba kibuyu boga mbao kisuaheli: nzumari [masahihisho zumari] [u. 63] Kifaa cha kukunia. Nusu nazi [masahihisho] hukuniwa kwenye chuma kama msumeno [masahihisho], wakati mkunaji hukalia kifaa.pande za mbao za kukaliwa huchongwa kutoka mbao mmoja & huweza kukunjwa. [michoro miwili, mmoja huonesha kitu kidogo mmoja] kisuaheli: mbuzi (maana halisi = mnyama mbuzi) / kisu cha porini kisuaheli huitwa "munde". Vingi vinatoka Ujerumani, ila hici ni vyembamba zaidi. [mchoro] Max amepokea picha mbili zilizotariziwa kwenye hariri yenye rangi ya giza kwa ajili ya kuninginizwa ukutani [u. 64]. Nilikuwa nimezinunua [?] pamoja na vitambaa vingine kwa Muhindi Tanga. Halafu kitambaa chepesi sana labda kutoka nyasi za nanasi kimetariziwa na vipepo kwa hariri nzito kitambaa cha mezani,kazi ya Wahindi. –" [Utafsiri]

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (62)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
  • unknown actor (Mnunuzi)
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka 1905-12-24
Maelezo
"43. Kijiko cha mbao Kijiko / Amani 24. mwezi wa kumi na mbili. 1905 / TB 46,62 / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 43
Scientific use:
Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: Haya nina picha nyingine hapa imesajiliwa hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18311_001 hebu ngalia unaweza kutambua ni kitu gani hicho? R: Hivi ni vijiko vilivyotengenezwa na miti I: Vijiko vilivotengenezwa na miti? R: Eeeeh I: Unaweza ukatuambia ni tamaduni za watu gani walikuwa wakitengeneza vijiko vya namna hiyo? R: Vijiko hivi tamaduni za watu waliokuwa wanatengeneza ni wapare, wachaga, ambao ndiyo najua kwamba walikua wanatengeneza I: Wapare na wachaga? R: Eeeh I: Kwa kipare vijiko kama hivi vilikuawa vinaitwaje? R: Miko I: Miko? R: Eeeh I: Na kichaga? R: Kwa kichaga siwezi nikajua I: Kipare ni miko? R: Eeeh ukiwa mmoja ni muko ikiwa mingi kama hapa ni miko I: Aaaah unaweza ukatuambia ni maeneo gani ni mikoa gani vitu hivo vilikuwa vikipatikana sana R: Mkoa wa Kilimanjaro I: Mkoa wa Kilimanjaro unaweza ukatuambia matumizi yake miko ilikuwa ikitumikaje? R: Ilikuwa ikitumika kwa kulia chakula I: Kulikuwa na chakula maalumu au vyakula vyote ulikuwa unaweza ukalia miko? R: Tuseme vyakula vyote hata makande, na wali, eeh I: Mapure? R: Eeeeeh mapure vitu vyote kinatumika kulia hivi I: Nani watu gani walikuwa wakitumia wajinsia gani? R: Wa jinsia zote I: Umri? R: Umri wowote maana ni kifaa chao cha familia wakati huo vijiko vya kizungu vilikua vinaitwa vijiko vya kizungu vilikua havijatokea kwahiyo wakati huo vilikua vinatumika hivi kwahiyo jinsia zote iwe ni mtoto mdogo mpaka mtu mwenye umri mkubwa anatumia bila shida yoyote kwenye família I: Kwasasa miko inatumika kwenye jamii ya wapare? R: Kwasasa nadhani inatumika kwa watu wachache sana kwasababu wameelimika saivi wanatumia vijiko vya kizungu I: Kwahiyo kutumia vijiko vya kizungu umeelimika hahahah R: Hahahaha I: Au tumepitwa na wakati tumeacha asili yetu R: Tumeacha asili lakini hatujaacha kabisa siunaona kijiko kama hichi kipo hapa ndani kwangu I: Kiko hapa ndani? R: Eeeeh I: Tutaomba tukione hahahaha unadhani inaweza ikafika wakati miko itakuwa haina thamani na haitumiki tena kwenye jamii za watu uliowataja? R: Eeeh inawezekana hivyo kwasababu kutokana na hali ya sasa hivi watu kwa kweli wanaweza wakawa wameacha lakini wale watu wa zamani wanapenda vitu kama hivyo I: Kilikuwa kina umuhimu gani kwenye tamaduni za watu wapare? R: Wapare? I: Ndiyo R: Kina umuhimu kwasababu mtu mwingine akishaona kitu kama hiki anavutiwa nacho na hata jinsi kilivo tengenezwa anaweza akajua kitu hiki kina matumizi yake ni vipi kwahiyo akavutiwa akaona akinunue eeh! I: Vinatengenezwa au kutokana na usasa tulio nao watengenezaji nao wameacha? R: Kutokana na usasa tulio nao vinatengenezeka lakini ni kwa watu wachache sana ambao ndiyo hivyo nakuambia umri wa miaka sabini na kuendelea ndiyo wanaweza wakavitumia lakini vijana sasa hivi hawawezi na wala hawazingatii kwasababu vimekuja hivi vijiko vya kizungu ndiyo wanavyo vitumia I: Na waliokuwa wanatengeneza hivyo ni wa jinsia gani wa kike au kiume? R: Wa kiume I: Sawasawa na unaweza kutuambia nyenzo au material yaliyotumika kutengeneza miko? R: Material waliyokuwa wanatumia walikuwa na visu vyao kwanza panga pili kuna visu ambavyo walikuwa wanavitumia kwa kutengenezea huu mduara eeh I: Na hiyo miko yenyewe ni nyenzo gani ni material gani? R: Miti wanatumia miti I: Ni miti aina gani ilikuwa ikitumika Zaidi? R: Miti iliyokuwa ikitumika ni miti kuna baadhi ya miti ambayo walikuwa wanapendelea kuitumia ambayo hata mwanadamu akila mizizi yake haiwezi kumdhuru eeh kwahiyo miti iliyokuwa inatumika ni miti ambayo haidhuru I: Unaweza ukaifahamu jina labda jina la hiyo miti? R: Kwa kweli nakumbuka mti mmoja tu ulikuwa unaitwa Mriringwi I: Ulikuwa unaitwa? R: Mriringwi kwa Kipare lakini I: Sawasawa kutokana na design ya aliyetengeneza hiyo miko ikiletwa kwa sasa na wewe ni muumini wa miko hahha ikaweka sokoni utanunua kwa shilingi ngapi? R: Nitakimbilia kweli hata kwa shilingi elfu tano mmoja ntanunua kwasababu hata huu unaosema hapo nilileta sasa kwasababu waliona ni kitu gani nilinunua kila mmoja kwa shilingi elfu mbili nilinunua kwa wakati huo elfu mbili lakini sasa ndiyo hivyo I: Ulinunua wapi? R: Nilinunua kule kule kijijini kwetu I: Unaweza ukatutajia maeneo uliponunulia kama ni soko basi soko gani? R: Nilinunua same sehemu za mlimani huko upareni tuseme ni upareni sehemu moja ya vudee ndiyo nilinunua I: Vudee? R: Eeeeh I: Kwahiyo leo nikienda vudee nikisema miko siwezi kuikosa? R: Utaipata I: Hivi vudee unapita hapa same? R: Unapita same unaelekea mwembe I: Mwembe nimefika R: Umefika mwembe? I: Eeeeh unapanda kule juu kule kama unaenda shengena R: Very good sasa kule miko kama hii unaipata sisi kijiji tunachokaa kuna babu mpaka saivi anatengeneza eeh

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview. No. 07
mwandishi: I: Mohamed Seif (NIMR), R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-08-19, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (132)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (62)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Kisu kichaka

Kisu kichaka

r 2018 / 18293
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kipasulio cha nazi, Mbuzi

Kipasulio cha nazi, Mbuzi

r 2018 / 18424
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Sanduku la ugoro

Sanduku la ugoro

r 2018 / 18431
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Chanuo la mbao

Chanuo la mbao

r 2018 / 18493 a
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Chanuo la mbao

Chanuo la mbao

r 2018 / 18493 b
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Chanuo la mbao

Chanuo la mbao

r 2018 / 18493 d
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Filimbi ya mbao

Filimbi ya mbao

r 2018 / 18504
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kijiko cha kuchochea cha mbao

Kijiko cha kuchochea cha mbao

r 2018 / 18506 b
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kijiko cha mbao

Kijiko cha mbao

r 2018 / 18303
Rejeo la ndani la kitu
Kitu kinacholingana

Rejeo la ndani la kitu

Löffel - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt

Esslöffel - Staatliche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:36:58+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji