Wakati
2023-06-14
Maelezo
I: Sawasawa haya tunaendelea na picha nyingine hapa nina picha imesajiliwa kwa namba 2018_18426_C hebu angalia picha hii unaweza kutuambia hicho ni kitu gani?
R: Haya ni makoja
I: Makoja?
R: Eeeeh yanaitwa makoja
I: Makojaa ni kilugha gani hicho?
R: Kisambaa
I: Mnaita makoja?
R: Eeeeeh
I: Makoja?
R: Eeeh yanavalishwa shingoni haya unavalishwa linazungushwa unavalishwa linazungushwa kama mara tatu hivi utakuwa unapendeza
I: Wanavalishwa watu gani?
R: Mara nyingi wanaotaka kuolewa
I: Wa kike?
R: Eeeeh wanawake makoja ya wanawake
I: Wanawake?
R: Eeeeeh
I: Kuanzia umri gani?
R: Kuanzia miaka 18 akipata mchumba akiozeshwa anatafutiwa makoja kwa ajili ya ndoa eeh na anavalishwa
I: Kwahiyo inavaliwa wakati anataka kuolewa?
R: Anataka kuolewa eeh
I: Kipindi ambacho anawekwa ndani au wakati anatoka?
R: Anawekwa ndani akitoka sasa kwenda kwa mume wake anavalishwa anapambwa anaenda kwake
I: Ni wasambaa tu peke yake wanatumia makoja au na makabila mengine pia walikuwa wanatumia?
R: Kwa ninavyoona makabila mengine pia yanatumia kwasababu wamasai wana shanga nyingi sana lakini msambaa hana nyingi sana yeye ana makoja eeh
I: Kwahiyo msambaa ni makoja?
R: Eeeeeh
I: Lakini hiyo inaonekana ni kabla ya kupatikana kwa shanga au kipindi hiko shanga zilikuwepo hebu tuambie?
R: Kipindi hiko shanga kulikuwa hakuna ni makoja tu
I: Makoja tu?
R: Eeeeeh
I: Kwahiyo ni wasambaa na wamasai?
R: Wasambaa, wazigua, wabondei walikuwa wanaendana mambo yao karibu yanafanana fanana mengi sana
I: Wote walikuwa wanavaa?
R: Eeeeh
I: Na makabila haya yanapatikana sana mikoa gani?
R: Mkoa wa Tanga
I: Mkoa wa Tanga?
R: Eeeeh
I: Sawa unaweza ukafahamu mkoa wa tanga sehemu gani hasa yalikuwa yakivaliwa makoja tuelezee?
R: Zamani kulikuwa kuna miviga huko mtu anaingizwa kwenye miviga akiwa anatoka kwenye miviga makoja yake anaozeshwa anaenda kwake yuko vizuri
I: Sawa na ukilinganisha na sasa makoja yanaendelea kutumika au unadhani ikafika kipindi makoja?
R: Wala hayajulikani kwanza
I: Ndiyo
R: Vitu vya zamani havipo kwanza saivi humkuti mtu ana mtoto anawekwa ndani sijui achezewe mviga hamna iliisha hiyo
I: Iliisha?
R: Eeeh saivi ni utandawazi
I: Hahahahahha sasa hivi ni utandawazi?
R: Eeeeh ni utandawazi
I: Makoja yalikuwa yanavaliwa na watoto wa kike tu?
R: Eeeeh wanawake has pale anapotaka kuolewa
I: Kuolewa?
R: Eeeeeh
I: Kashawekwa ndani?
R: Eeeeeh
I: Na walikuwa wanawekwa muda gani ndani?
R: Alikuwa anawekwa mwezi mmoja kadri ya uwezo wa wazazi maana kule kutengenezwa mtajiandaa wengine miezi miwili kadri ya uwezo wa wewe utakavo hudumia wale watu kwahiyo kila mtu itategemea uwezo wake
I: Sawasawa kwahiyo sasa hivi makoja hayapo?
R: Sasa hivi baba hayapo kwanza muda wa kuwekwa huko ndani uko wapi mtu akitokala kwanza la saba, form four, form six yuko wapi atakaye vikwa koja akaendani angoje koja hayupo
I: Hakuna?
R: Hapana
I: Sawasawa kwahiyo sasa hivi wasambaa hawatumii tena makoja?
R: Tena huo mviga unaweza ukae hata miaka 20 hujasikia mviga hakuna
I: Mviga ni nini?
R: Ndiyo hizo ngoma za mtoto wa kike
I: Ambazo ndiyo zakuweka watu ndani?
R: Eeeeh wanawake watoto wakike
I: Mviga?
R: Eeeeh mviga
I: Kwahiyo hata saivi mviga hakuna?
R: Hakuna
I: Kwanini miviga hakuna tena hivi sasa?
R: Watu wameendelea
I: Wameendelea nini? Hahha
R: Hahahhaha ya kale hayapo
I: Hayapo ya kale?
R: Hayapo
I: Hhahahaha sawasawa na waliokuwa wanatengeneza makoja ni watu gani hasa wakati huo wa zamani?
R: Ni wale akina mama eh
I: Wakina mama kuanzia umri gani?
R: Watu wazima wale ambao watawaweka ndani ndiyo wanachukua hizo shanga maana hayako duara yamekaa mabapa bapa ndiyo hayo wanayashona wanayafunga wanawavisha kipindi wanaolewa
I: Walikuwa wanaotengeneza ni kuanzia miaka mingapi?
R: Wakina mama watu wazima wale
I: Kwasasa unaweza ukakadiria walikuwa wanaanza kutengeneza kuanzia miaka mingapi kama unakumbuka?
R: Ilikuwa ni kuanzia miaka 45 na 50
I: Kwanini walikuwa watu wazima?
R: Kwasababu watu wazima ndiyo wana hekima kwenye mtu mzima hapa haribiki neno hapana ngumi hapo
I: Ndiyo hahaha
R: Hhahahah
I: Sawa sawa na unaweza kutuambia vitu vilivokuwa vinatumika kutengenezea makoja yanatengenezwa kwa kutumia kitu gani?
R: Makoja
I: Angalia vizuri unaweza ukatambua kwa kuangaliam picha yalikuwa yanatengenezwa kwa kutumia nini makoja?
R: Haya mara nyingine yalikuwa ni vigongo hivi vizuri ambavyo vinarembwa vinakatwa katwa vinatobolewa vizuri vinapendeza
I: Kwa maana ya miti?
R: Eeeeh
I: Vinatobolewa?
R: Vinatobolewa vinashonwa, vinatungwa na unavaa
I: Vilikuwa vinatungwa na nini?
R: Yani vikikatwa katwa vizuri na kutobolewa njia basi unachukua kamba na kama yenyewe niya mti
I: Kamba niya mti?
R: Eeeh unachubua mti inakuwa vizuri unachomeka kwenye matundu anavishwa akitolewa hapo anakuwa kapendeza sana
I: Ni mti gani hasa ulikuwa ukitumika kupata vitu vya kukatia mti kupata hivi vipande vidogo vidogo na kamba yake?
R: Ni vya kamba kuna mti unaitwaje sosokole, sosokole una kamba
I: Sosokole?
R: Sosokole eeh unakamba ngumu hata kwa kujengea unajengea haukatiki kwasababu una Kamba mgumu sana
I: Ndiyo
R: Kwahiyo hiyo inachukuliwa inatungiwa wasichana wanavishwa kwenye shingo
I: Na hadi kipindi ambacho zimepotea zilikua zinatengenezwa kwa kutumia hivyo hivyo miti pamoja na kamba za sosokole au ilifika wakati ikabadilishwa vitu ambavyo vya kutengenezea vikabadilika?
R: Ndiyo sasa hivi vimebadilika ndiyo zipo hizo shanga sasa
I: Shanga?
R: Eeeeh sasa hivi hivyo havipo hizi ni shanga sasa vinaenda kimtandao hahahah
I: Eeeeeh
R: Viko kisayansi zaidi vimeboreshwa zaidi
I: Ndiyo sawasawa kwahiyo saivi shanga?
R: Ni shanga
I: Labda umesema inaitwaje?
R: Makoja
I: Mkoja ukiletwa kwenye masoko ya sasa hivi unafikiri inaweza ikauzwa shilingi ngapi?
R: Sasa nani atanunua mkoja wakati kuna shanga hahahahhaha
I: Hhahahhahaha
R: Labda uganga hahahhah
I: Hahahahahah labda za uganga
R: Eeeh uganga kama umeambiwa ukatafute koja ndiyo ukalitafute sasa lakini sasa ukute dukani linauzwa alafu unakuta vya ndani vimetengenezwa mishanga yafanya kumeremeta huwezi ukalichukua
I: Huwezi ukalichukua
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 18
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali