"Jumapili 27. Mwezi wa kumi na moja 1904 [imepigwa mstari] Leo asubuhi nimepokea mapambo kadhaa ya ki-Massai: 7. Bangili yenye pande mbili ya pembe mwishoni imepambwa na shaba mwekundu na nyaya za shaba ina manyoya ya kanu (= 1 Rupie) [mchoro] eneo: Stuhlmann. Mit Emin Pascha ins Herz von Afrika, Berlin 1894 kitabu 1 u. 51 / picha angalia: Fischer, G. A. Das Maßailand. Mwezi wa tisa. Abz. aus d. Mitteil. der Geograph. Gesellschaft in Hamburg 1882-83. Hamburg 1885. Kibao 6 mchoro 1. / 8. Mkanda wa ngozi uliopambwa Huvaliwa kifuanishangaa buluu& nyeupe, ngozi imepakwa udongo mwekundu (= 1 Rupie) [mchoro] [...]" [Utafsiri]
chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 43 (103) mwandishi: Karl Braun
„8. Mkanda wa kiunoni wa Massai/e mairenai [?] /huvaliwa kifuani una shanga za buluu na nyeupe, umetengenezwa na ngozi iliyopakwa matope mekundu /Amani 27. mwezi wa kumi na moja 1904 = 1 Rp / Merker, M. Die Masai, 1910, u. 143-144 / TB 43,103 / [mchoro]" [Utafsiri]
chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566 mwandishi: Karl Braun
Nambari za hesabu za zamani
8
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).
chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.
I: Nina picha nyingine hapa ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18202_1 bibi […] hebu iangalie hii ulisema inaitwaje hii?
R2: Sasa hii naona tena imeshonwa na ushanga hii ni engosokwani anavaa hapa
I: Anavaa wapi?
R2: Shingoni na wanavaa vijana
I: Engesokwa?
R2: Eeeeh maana hii ya kale kama hii ya kwetu ya kisasa yani anashonea kila mahali siyo mahali moja tu unapitisha sasa hivi unazungushia mpaka mwisho hapa lakini hii niya kale eeh engosokwani
I: Na ilikuwa inatumika kuvaa shingoni?
R2: Eeeeh
I: Kwa vija wa jinsia gani?
R2: Hawa vijana morani wanavaa siku ya sherehe wanaweka shingoni anaenda kwenye ngoma kucheza
I: Kwenye ngoma ndiyo anavaa hiyo?
R2: Eeeeh
I: Kwa ajili ya kuvutia?
R2: Eeeh
I: Sasa hivi wanazitumia bado Engosokwani bado mnazitumia sasa hivi katika jamii yenu hii ya kimasai?
R2: Inatumiaka ya ambira siyo ya ngozi siunaona hii ni ngozi siunaona ipo ngumu sana ya nyati we siunajua nyati ile ambayo ina mapembe mbogo eeh sasa zamani watu walikuwa wanapata ngozi ya mbogo sasa hivi nani anaua mbogo labda kama anashonea ya ng’ombe lakini hii ambayo ni nzito namna hii niya mbogo ngozi ya mbogo ndiyo inaitwa engosokwani kwa kabila la kimasai
I: Kwahiyo mbogo ndiyo anaitwa Engoswaki?
R2: Eeeh
R1: Sasa kutengeneza hii ndiyo wanaita engosokwani maana kwa kimasai mbogo anaitwa Engosokwani
I: Na aliyekuwa anavaa hiyo kuna kitu kingine alitakiwa kukivaa pia?
R2: Anaweka nyingine ambayo ipo hapa alafu anasimama nani yake hapa
I: Nini?
R2: Inaitwa Emajira anavaa shingoni yote
I: Kwahiyo umuhimu wake mkubwa ilikuwa nikupendezesha tu mtu?
R2: Eeeh kupendezesha mtu urembo
I: Na sasa hivi hamtengenezi kama hizi?
R2: Hatutengenezi lakini kama mtu anataka anashona lakini niya ambira au kama atasema nitengenezee ya ngozi lazima nishone tu maana najua kuitengeneza
I: Lakini kama mtu hajataka huwezi ukaitengeneza?
R2: Hapana
I: Matumizi yake yamepungua sasa hivi
R2: Yani hiyo niya watu wa kale sasa hivi hakuna wanaopenda watu wa kale ndiyo wanapenda hawa watoto wa kisasa wa shule hakuna tena wao wanaendelea na usasa na mambo ya kisasa siku hizi
I: Na wanaotengeneza hizo ni akina mama pia?
R2: Ni wakina mama hakuna kitu ambacho anatengeneza mwanaume hapa vyote hivyo vinatengenezwa na wakina mama
I: Kwahiyo maswala ya ushanga yote ni akina mama?
R2: Ni wanawake tu
R1: Wanavaa lakini wanaotengeneza nikina mama
I: Kwahiyo sasa nyie mnatofautishaje vitu ambavyo wanavaa akina baba na wanaovaa akina mama?
R2: Ipo wazee wa kale ambao wapo hapa hawavai wao na ina utofauti
I: Na umesema ni ngozi ya Mbogo na Emustani?
R2: Eeeh Emustani siunaona?
R1: Hii inavalishwa kwenye shingo
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. mwandishi: I: Mohamed Seif, R2: Anonymous
Mtu
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
Mnazi
Scientific use:
Wakati
2023-10-03
Maelezo
I: Asante nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18362_1 hii na ile ya kwanza ina utofauti?
R3: Haina utofauti, tofauti yake hii kuna ndogo alafu kuna kubwa inaonyesha kwamba ilikuwa niya watu wakubwa na vijana wadogo ila yote hii ni ndalama ninavoangalia mimi ni ndalama ileile
I: Hiyo ni ndefu kidogo kama unavyoiona hiyo ni ndefu kidogo
R3: Ina tofauti si ndiyo hizi hapa ndalama hii pia wanawekaga hapa mkononi
I: Hiyo ya kuvaa mkononi?
R3: Eeeeh siyo hapa ni hapa kwenye mkono wa juu inaitwa Arkataa
I: Kwahiyo hii ni arikataa?
R3: Eeeeeh
I: Lakini ni hiyo hiyo Ndalama?
R3: Eeeeh
I: Lakini niya kwenye mkono wa juu?
R3: Hii niya kwenye mkono ndiyo maana wanatofautisha arikataa na ndalama
I: Kwahiyo arikataa maana yake niya mkono wa juu?
R3: Eeeeh maana naya hapa ina jina lake naya hapa yenyewe ina jina lake eeeh kwahiyo zina majina mbalimbali
I: Na hii arikataa ya kwenye mkono wa juu walikuwa wanavaa jinsia gani ni wanawake au wanaume namba moja?
R1: Wanavaa wanaume na wanavaa na wanawake
I: Kitu gani kilichokuwa kinatofautisha arikataa ya wanaume na wanawake katika jamii yenu ya kimasai?
R1: Wanatofautisha maana ya wanawake wanashona na kuna kiungio ambacho wanaweka alafu inakuja kushika hii hapa eeh lakini ya wanaume haiungi hiyo ndiyo tofauti yake kati ya wanaume na wanawake
I: Wanaume hawaweki?
R1: Hapana
I: Na waliokuwa wanatengeneza hizi pia ni jinsia gani ni wanaume au wanawake katika jamii yenu ya kimasai?
R1: Wanawake hii ni kazi ya wanawake
I: Kwahiyo kazi za shanga zote ni kazi za wanawake?
R1: Eeeeh
chanzo: Amani-Stade Project / Massai Field Research 2023 / Interview No. 07 mwandishi: I: Mohamed Seif, R1-3: Anonymous
Mtu
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
Longido
Nyalaka
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1905-03-14, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 44 (82)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566 (8)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1904-11-27, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 43 (103)jifunze zaidi
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:01:46+01:00
Maoni
Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.