Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/3

Kofia nyekundu

Sammlung Braun
r 2018 / 18369
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18369
Kichwa
Kofia nyekundu
Nyenzo
Nguo
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_c4fb1056-d9c9-45cd-99c8-24dbfec3a9ef
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Nguo/Vitambaa  
Uzalishaji
Wakati
mpaka ca. 1909-04-10
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Kununua / Uuzaji
Wakati
1909-04-10
Maelezo
"Jumamosi 10. Mwezi wa nne 1909 [imepigwa mstari] Asubuhi nimeendelea kuufanyia kazi mzigo mkubwa wa mimea kwa ajili ya Berlin. Mchana mafaili. – Najaribu kukusanya vitu vyote ambavyo Wasuaheli [sic] huvinunua kwenye maduka ya Wahindi kama mahitaji yao. Kwa lengo hilo nimewafanya akina „Boy“ waandae orodha kwanza na hapo nikakuta vitu vingine ambavyo hata sivijui. Leo nimepata :kofia ya kituruki yenye rangi nyekundu iliyopauka imetengenezwa na kitambaa gandamizo chekundu huitwa kwa kisuaheli: kofia stambuli huku juu ina mpini mdogo [u. 46] inasemekana kwa kibonei [?]: huitwa shuju [?]. Kofia ya aina hiyo hugharimu hela 50 hapa Amani. Tanga hununuliwa kwa hela 25. Pia nikanunua kofia nyeupe ya kawaida. Imetariziwa na nyuzi nyeupe aina hii huitwa kofia ya eherhani [?] [inadhaniwa r 2018 / 18373]. Maana yake kofia iliyotengenezwa kwa cherehani. Hapa moja inagharimu nusu rupie, kule Tanga kama hela 30. / kofia kama ile yenye jina hilo hilo ila imeshonewa upinde wenye mapambo ya nyuzi nyeusi hapa inagharimu hela 75 pale Tanga hela 50 Mapambo hapa [?] kwa N* [1] ni mistari inayoingiliana vimeshonwa kiholela kwa mashine [michoro mitatu yenye umakini ya mistari ya mshono] Ikiwa kofia imekeketwa huitwa kofia ya someno [?], kofia iliyoshonwa [?] kamwe si laini kofia ya futo / kofia maridadi na ya thamani huitwa kofia buibui (shajara 52, u.39) na hulipiwa Rupien kadhaa. Pia nimenunua nguo kadhaa: [u. 47] [mchoro wa rangi] Kitambi, kitambaa chenye rangi nyingi kilichofumwa. Hutengenezwa India au inawezekana Uingereza. Mistari yenye rangi nyingi hutengenezwa na mapambo ya nyuzi zenye rangi zilizofumwa. Rangi kuu ni zambarau tepe nyembamba zenye rangi ya machungwa – manjano, nyeupe rangi ya ndimu nyeupe nyekundu na nyeupe zimefumwa kwa pambo lililopo hapa kila mstari hutengenezwa kwa nyuzi mbili. [mchoro wa rangi] pambo la juu huchukua nusu ya upana wote na linajirudia upande mwingine [?]. upana wote ni 106 cm, urefu 212 cm. Bei hapa Amani ni 1 rupie. Kitambaa huvaliwa na wanauma kiunoni. Kitambi kingine upana 16 cm b 168 kina upinde mwekundu katikati kuna sehemu zilizozungushwa na nyuzi za manjano, zenyewe ziliundwa kwa nyuzi nyekundu na nyeusi [?]. Kati ya upinde mwekundu na eneo la ndani kuna / [u. 48] [mchoro wa rangi na mwandishi] mstari wa wima mweupe. Kitambaa hicho pia huvaliwa na wanaume kiunoni na moja hugharamia 1 rp. 25. / Shuka au kitambaa cha kiunoni na upinde wa kawaida mweusi na mwekundu. Urefu 172 upana 89 cm, bei hapa Amani hela 60. [mchoro mdogo wa rangi] / shuka ya kawaida zaidi linagharamia hela 50 ni kitambaa, upana 98cm na urefu 186 cm lang. Upinde ni [masahihisho] mistari mwekundu kijani na zambarau. Bei ni hela 50. [mchoro mdogo wa rangi] / Pia nimepata ubani tofauti tofauti: [...] [u. 50] [mchoro wa rangi] pana [...] [?] (shajara 52, u. 59) Kikoi kina upinde wenye rangi nyingi. Vitambaa hivi vinasemekana kuwa maridadi zaidi. upana 95 cm urefu 168 cm bila upinde wa nyuzi zinazoning‘iniya urefu wa hizo ni 10 cm." [Utafsiri] [1] The N-word (N*) is a highly racist term used to refer to Black people. The term originated in the context of "racial" theories and is closely linked to the history of slavery and colonialism. In the transcription of original sources, it has not been reproduced but instead marked as a racist, derogatory, and offensive term.

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (45)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • Mtu, haijulikani (Mchuuzi)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
ca. 1909-04-10 - 1909-04-10
Maelezo
"124. Kofia nyekundu ya Boy's5 / Kofia nyekundu [?], Kofia Stambuli / Amani 10. mwezi wa nne 1909 = hela 50 (kwa wazungu!) 25 " (kwa waafrika!) / TB 53,45. / mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 124
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-06-08
Maelezo
I: naomba nikubadilishie picha, nimeshka picha imesajiliwa 2018_18369_001, hebu angalia hiki ni kitu gani R: hii ni kofia, kofia hii ilikuwa inaitwa kitunga I: manake ni nini na kwanini iliitwa kitunga R: ni jina tu kutokana na haka kajiurembo ka hapa juu ndio ikaitwa jina hilo kitunga I: na ilikuwa inapatikana zaidi maeneo gani katika nchi yetu ya tanzania R: lilikuwa ni vazi la watu wa pwani, islamic I: unaweza ukatutajia ni mikoa gani R: ni mkanda wa coast wote, na kigoma kule islamic wamekaa, na wakati huo mtu akivaa kofia hizi uh! akiingia mahali lazima watu wasimame I: kwa nini R: kila zama wana mambo yake, ilikuwa ndio mavazi ya hadhi I: kwa hiyo mtu akivaa hiyo inakuwa ni mtu mwenye hadhi kubwa, ila sio mtu yeyote alikuwa anaweza akavaa hiyo kofia R: hapana, una habar zamani hela ilikuwa iko chini na kuna baadhi ya vitu... na wakati huo pengine utakuta bei yake ni senti tano, lakini huyo anayepata senti 5 mpaka anainunua lazima akuambie yanazungumzika, na wengine wlikuwa wanavaa kutokana na uwezo wa uchumi wao I: kwa hiyo kitunga kilikuwa kinauzwa kwa gharama kubwa kidogo kwa kipindi chicho R: ee I: na ilikuwa inavaliwa kipindi gani R: ndio nimekuambia ni vazi la watu wa pwani haswa islamic, I: ilikuwa ni kwenye matukio maaluma au ni muda wowote mtu anaweza akavaa R: ni muda wowote, lakini mavazi yake kitunga wewe leo huwezi kuvaa na suruali ya kuchonga, hii lazima upate kanzu na koti I: koti la namna gani R: koti la kawaida, halafu ilikuwa raha yake saa nyingine ilkuwa iweke upande I: kwa hiyo mtu anayevaa kitunga lazima avae kanzu na koti katika muonekano R: ni katika muonekano tu I: labda ilikuwa na masharti ya aina ya viatu pia maana kuna baadhi ya vazi huwezi ukavaa kanzu R: kipindi cha matumizi kama hivi likuwa viatu vyake vikubwa ni makubadhi, viatu vya wazi I: na kitunga kwa hali ya sasa kinatumika R: ah, tunakiona lakini kwa umbali sana, halafu kuna baadhi ya vijana wakikuta vya marehemu babu zao wanavaa kama fashen lakini sio vinavaliwa kuwa ni vazi, enzi yake imepita I: nayo haiwezi ikarudi R: sio rahisi I: kwa nini sio rahisi R: unajua sasa hivi tunakokwenda...lakini kuna siku moja nilisema ifike wakati hizi tawala kuna vitu lazima waviangalie, kwa mfano kama sasa hivi ukifungulia tv unaambiwa oh sijui maji lakini nani wa kulinda maji, mimi nilitegemea mama samia tangia ameingia madarakani leo ilikuwa akemee wasichana wanaotembea uchi, yeye kwa vile ni mwanamke ilikuwa aone uchungu na akemee, sasa mama nini utakaoyatengenezwe na yatatengenezwa vipi, anakuja makamu wa rais kuna kuja watoto wa shule wanafunga migomba uchi tunamuona, sasa hayo maadili mnayoyataka ni yapi, serikali kwanza ikae iangalie kama inataka irudishe mfumo wa maadili, serikali ndio isimamie hili, mimi ninasema hata kwenye mataasisi ya dini pia inachangia kuharibu maadili, mimi kwa umri wangu nilishaona ukristo wa nyuma, unakuta mtoto wa kikristo anaenda kanisani mwili wake unamtosheleza kabisa kwa nguo anajua anakwenda mahali pazuri patakatifu, unaangalia wale mabinti I wanaokwenda kwenye ibada halafu naked kabisa na mchungaji unasimama unaangalia unazungumza huku mate yanakutoka, kwa nini hukemei vitu kama hivi, kwa hiyo hizi zama z maadili zilishapita I: kitunga bado kinatengenezwa hivi sasa R: watumiaji hawapo, utengenezaji wake pia... I: umepungua au umeisha R: itakuwa umeisha I: kwa hiyo leo hii mimi nikihitaji kitunga... R: unaweza ukakipata bangladesh huko kidogo kinatumika I: na je kwa tanzania au vinginezo aagize au mtu aje nacho R: ee au mtu aje nacho I: na kwa tanzania kipindi hicho ni watu gani walikuwa wakitengeneza vitunga R: vilikuwa imported I: kutoka nchi gani R: huko huko bangladesh ndio kwenye ambako walikuwa wanakitumia sana, kilikuwa ni kitu cha biashara I: japo kilikuwa kinaingizwa kutoka nje, je unaweza ukazungumzia nyenzo zilizokuwa zinatumika kutengeneza kitunga R: kitunga ilikuwa ukikiangalia ni kama pamba iliyochatwa, lakini katika mchakato wa kitambaa sio pamba kama pamba, lakini imechakazwa katika mchakato wa kitambaa, ilikuwa ni kitu kama hicho I: kwa kipindi hicho umeseme kitunga kilikuwa ni kivazi cha thamani na chenye hadhi kwa anaevaa, thamani iliyokuwa inauzwa kipindi kile ukiileta katika maisha yetu ya sasa, inaweza ikawa ni shilingi ngapi R: kama elfu 5 au elfu 10 kitu kama hicho

chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023 / Interview No. 02
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Amani
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1906-06-04, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 47 (44)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-25, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (36)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (43-50)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-08-23, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (56-57)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1908-07-30, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 52 (39-40)jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Tarehe ya kutengenezwa: 1909-04-10, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 53 (45)jifunze zaidi

Rejeo la ndani la kitu

Kofia nyeupe yenye tarizi

Kofia nyeupe yenye tarizi

r 2018 / 18373
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na
Kofia nyeupe yenye tarizi nyeusi

Kofia nyeupe yenye tarizi nyeusi

r 2018 / 18385
Rejeo la ndani la kitu
Kuhusiana na

Rejeo la ndani la kitu

Kofia (Fes) - Staatlche Museen zu Berlin

Rejeo la ndani la kitu
ist ähnliches Objekt
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:52:05+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji