Hinweis: Um die korrekte Darstellung der Seite zu erhalten, müssen Sie beim Drucken die Hintergrundgrafiken erlauben.
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
Slider Bild - CC BY-NC-ND 4.0
1/4

Bomba lenye muundo wa kichwa cha udongo wa mfinyanzi

Sammlung Braun
r 2018 / 18368
Taasisi inayotoa
Museen Stade
Eneo la Mkusanyiko
Sammlung Braun
Nambari ya uvumbuzi
r 2018 / 18368
Kichwa
Bomba lenye muundo wa kichwa cha udongo wa mfinyanzi
Vipimo
Urefu: 27cm
Nyenzo
Mbao,
Kauri
Kiungo cha dondoo
https://www.amani-stade.gbv.de/item/sw_ms_c77282c3-30d8-4f5f-ad3b-41ba13a01c12
nakala kwenye ubao wa kunakili
Kikundi cha kitu / kitu cha mtu binafsi
Kitu cha mtu binafsi
Uainishaji
Vyombo vya kuvuta sigara  
Uzalishaji
Wakati
mpaka 1906-04-15
Mtu
  • Missionsstation Hohenfriedeberg (Mteja)
  • Mtu, haijulikani (Mtengenezaji)
Mahali
  • Mlalo
Kununua / Uuzaji
Wakati
1906-04-15
Maelezo
„Jumapili 15 mwezi wa nne 1906. [imepigwa mstari] [...] [?] tumeahidiwa na Bwana na Bibi v. Horn [...] [?]. Walikuja [...] [?] saa 6 na pamoja nao Bwana W. Bock. Asubuhi niliandaa mapambo ya maua [...] [?] na [...] [?] Drachenburg: Sesbania grandiflora, Mina lobata, Cobaea scandens, Melaleuca leucadendron & imefunikwa na maua mekundu na rangi ya manjano [...] [?] Erythroxylon Coca. Wageni wetu wamewahi kufika na tumepitia pamoja masaa [...] [?] [...] [?] Saa 10 tumeachana tena [...] [?] Max & mimi tumekwenda [u. 118] kutembea kidogo & jioni tulikuwa wavivu. – Kupitia BiBi v. Horn [?] nimepata viko vitatu vya pekee sana vimetengenezwa kwa udongo mweusi na mdakalo wa mbao: [mchoro] ndege kwa maneno ya msanii ni bata. Ninavyoona kutokana na umbile kiko hicho kinakosa mfuniko ambamo utepe wake wa kuunganishwa hukaa kwa nyuma[mchoro] wazo wa kiko hicho kinaweza kimetokana na palepale kama vile vilivyochorwa u. 82. Mdakalo umechongwa kipekee sana. [mchoro] mwanamke aliyelala (kila moja hela 10)" [Utafsiri]

chanzo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (118)
mwandishi: Karl Braun
Mtu
  • unknown actor (Mchuuzi)
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mnunuzi)
    GND Explorer
Mahali
  • Amani
Malipo
Wakati
kutoka 1906-04-15
Maelezo
“72. Kiko kutoka udongo mweusi / Mishonari. / mrija umechongwa kwa ubunifu hela 10 / Amani 15. mwezi wa nne 1906 /kazi ya Mlalo / TB. 46,118 / [mchoro]" [Utafsiri]

chanzo: Museen Stade, r 2018 / 18566
mwandishi: Karl Braun
Mtu
Nambari za hesabu za zamani
  • 72
Urithi
Wakati
1934-07-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1934, aliyekuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Biolojia ya Kilimo na Misitu (Biologische Reichsanstalt für Land- und Forstwirtschaft) Karl Braun (1870–1935) alitoa kile kinachoitwa “Kolonialsammlung Braun” (Makusanyo ya Mkoloni Braun) kwa Jiji la Hanseatic la Stade, au tuseme aliyekuwa mwakilishi wake, meya wa wakati huo Hans Arthur Meyer (1884–1961). Tazama faili „Uhamisho wa makusanyo ya kikoloni kutoka kwa diwani mkuu wa serikali Profesa Dk. Karl Braun huko katika Jiji la Stade” („Überlassung einer Kolonialsammlung vom Oberregierungsrat Professor Dr. Karl Braun in Stade an die Stadt Stade") katika Jimbo la Saxony ya Chini Hifadhi ya Nyalaka ya Stade (Niedersächsischen Landesarchiv Standort Stade).

chanzo: Niedersächsisches Landesarchiv Standort Stade, Dep. 10 Nr. 03025
Mtu
  • Braun, Karl (* 1870 † 1935) (Mfadhili)
    GND Explorer
  • Hansestadt Stade (Mpokeaji)
  • Hans Arthur Meyer (1884 - 1961) (Mpokeaji)
Mahali
  • Stade
Mkopo
Wakati
1997-02-17
Maelezo
Mnamo mwaka 1997, aliyekuwa mtunza kumbukumbu wa jiji kwa wakati huo Jürgen Bohmbach anahitimisha makubaliano ya makabidhiano kwa mkopo wa kudumu katika Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) chini ya aliyekuwa mkurugenzi wa wakati huo Gerd Mettjes kwa kutia saini. Baadaye, makusanyiko kutoka kwa Karl Braun yalihamishiwa kwenye Jumba la Makumbusho (Museumsverein Stade e.V.) kwa ajili ya utunzaji.

chanzo: Museen Stade, Vereinbarung Leihgabe "Brauns'sche Kolonialsammlung"
Mtu
Mahali
  • Stade
Scientific use:
Wakati
2023-09-07
Maelezo
I: kwa hiyo ulikuwa na akili ulijua kinachoendelea, sawa sawa, kwa hiyo hapo ni namba saba na namba nane, na nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18368_001, hebu anglia na hicho R: Huu sio msumeno I: Hapana hii ilikuwa imechanganywa na kitu kingine, tukaziba ili kibakie chenyewe R: Tuseme sana sana hapa kitu ambacho naona kidogo vinaweza vikafanana, ingawa hiki niseme huu mpini wake umeboreshwa I: Na hata hicho kichw chake pia ukikiangalia kinafanana na hivi ulivyoviona hiki cha namba saba na namba nane R: Hapana I: Unaweza ukaangalia hicho kichwa chake jinsi kilivyo, kinavyoonekana hivi R: Nikishika kwa huku mbele ndio kinaonekana hivi I: Eee R: Tena hivi labda niseme tu vinatumika na hawa viongozi kama wafalme I: kwa hiyo ilikuwa ni walfame ndio wanatumia R: Eee nilivyoona kw jinsi kilivyochongwa, ninaweza kusema kwamba hivi vilikuwa vinatumika kwa watu maarufu I: Sio wananchi wa kawaida R: Eee, au ni mti huu? I: kwa mujibu wa maelezo kwa hapa ni udongo wa mfinyanzi mweusi na zimetoka mlalo pia, hii ilinunuliwa siku ya jumapili ttarehe 15.04. 1906 R: Sasa unafahamu ndio yale tunayoyazungumza, inawezekana labda akaja mtu kutoka huko kuja kuuza huku akanunua, kuna hawa wamakonde não... I: Walifika lini wamakonde hapa? R: Hapana sijui, sana sana labda huko sehemu za bondeni inawezekana wakawepo hao watu lakini walifanya kuja… I: Walifanya kuja kukaa hapa R: Hapana I: Walikuja kwa biashara au? R: Labda inawezekana wakaleta kwa biashara I: Inawezekana nako pia kuna udongo wa mfinyanzi, maana inavyosemekana mlalo ni mlesa tu maarufu kwenye udongo wa mfinyanzi R: Eee hapo ni sawa I: Kwahiyo hiki hujawahi kukiona? R: Hapana sijawahi kukiona

chanzo: Amani-Stade Project / Mlalo Field Research 2023, Interview No. 09
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mlalo
Scientific use:
Wakati
2023-09-09
Maelezo
I: Sawa sawa, ngoja tujadili tena picha nyingine, nina picha nyingine imesajiliwa kwa namba 2018_18368_001, hebu angalia unaweza ukatuambia ni nini hicho? R: Hiki nacho ni ‘Kiko’ lakini kimerembeshwa zaidi kulikoni kile cha kwanza, unajua mtu akianza kutengeneza ‘Kiko’ cha kwanza atakapotengeneza ‘Kiko’ cha pili ni tofauti na kile cha kwanza atakuwa amepata ufundi zaidi, anakiweka mapambo zaidi ili kuvutia wavutaji I: Labda tuangalie kile cha kwanza mdomo wake ni mfupi kidogo wa kuwekea tumbaku ukilinganisha na hicho ulichoshika, unadhani ni kitu gani kilepekea vikatengenezwa tofauti kwenye mdomo wa kuwekea tumbaku R: Unajua hawa mafundi wanadizini wenye kuvutia hao wanunuzi, naona wanatengeneza kutokana na wakati, hiki kimefanyiwa maringo zaidi lakini uso ni ule ule I: Ukiangalia hapo mbele kinaonekana kama kina sura ya mtu, unaweza ukahisi ilikuwa sababu gani kuwekea sura ya mtu kwenye hicho kichwa cha kuwekea tumbaku R: Hapo ninaweza kusema kwamba hiki kitu kinatumika kuvutwa na mtu ndio sababu kina sura ya mtu ndio kwa sababu kna sura ya mtu, wao wanatengeneza sura ya mtu kutokana na ufundi wao, maana hata ukiangalia unaona hiki na hiki kinakwenda sawa sawa kwa nini, kwa sababu hapa ni pembamba na hapa napo ni pembamba lakini ni tofauti, huu ni ufundi wao wanadizaini wenyewe hawa wahunzi I: Ukikiangalia unaweza kusema ni nyenz ganizilitumika kutengeneza hicho R: Huu ni mpingo huu, maana unaona wamekwaruza kwaruza hivi, hiki cha udongo hakina mpango zaidi kulikoni hiki, ndio kina maringo zaidi kulikoni hiki, kwa hiyo hii ni ya kumvutia mvutaji I: Kwa hiyo hii ni ya kumvutia mvutaji R: Eee I: Kwa hiyo inawezekana ilikuwa ni mti wa mpingo R: Inawezekana ni mti wa mpingo, maana mpingo hauungui ukiweka mkaa hivi hauungui kabisa I: Sawa sawa, na labda ukiangalia huo mrija wa kuvutia unaweza ukawa ulitengenezwa kwa mti gani? R:Mimi naona kuna miti fulani ambayo ina nafasi katikati, inakuwa kama bomba I: Unaitwaje huo mti R: Kama muanzi, kuna miti fulani ambayo ukiuchonga huku juu huko ndani kuna njia, kwa hiyo unafanya kuchokoa na kijiti I: Sifa yake ni mgumu au ni mlaini R: Ni mgumu,mpaka upige chini ndio upasuke I: Na ukilinganisha na kile ‘Kiko’ cha kwanza, kwahicho ulichokishika unadhani kikiletwa sokoni leo hii kikakutana n mvutaji R: Hiki ni imara zaidi kulikoni hiki I: Hiyo kamba yake tunaiona ni tofauti na ile ya kwanza, unadhani hiyo inaweza ikawa ni kamba ya aina gani R: Ni kama kamba ya manila ile nyembamba, lakini kufunga hivi ni kwa sababu ya kuimarisha huu ‘Mtemba’, hapa na hapa na hapa kwa ajili ya kuimarisha I: Kwa hali ya sasa kingeuzwa shilingi ngapi hicho ulichokishika R: Hiki hapa kwa wakati huu, hata shilingi elfu kumi unaweza ukauziwa maana ni kizuri zaidi, lakini sasa kwa wakati huu hakitakua na bei kwa sababu havitumiki I: tu assume umekutanan na mtu ambaye anatumia ‘Kiko’ kungekuwa tayari kulipa hiyo shilingi elfu kumi R: Anganipa hiyo shilingi elfi kumi kwa sababu amezoea kuvuta kwa kutumia ‘Kiko’

chanzo: Amani-Stade Project / Mlalo Field Research 2023, Interview No. 05
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mlalo
Scientific use:
Wakati
2023-09-09
Maelezo
I: Sawasawa basi asante ngoja tukupe picha nyingine sawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18368_001 hebu angalia picha hii unaweza ukatuambia ni kitu gani hicho? R: Hii si huo huo ‘Mtemba’ I: Unaweza kutuambia utofauti kati ya ‘Mtemba’ huo na tuliotoka kuujadili hivi sasa? R: Hakuna kubadilika ni hiyo hiyo I: Ukiangalia huu mti wake? R: Kamba ndiyo hiyo hiyo I: Na mti wake mbona unaonekana ni tofauti na ule? R: Unatengenezwa kwa kila namna leo wanatengeneza hivi kesho wanatengeneza hivi basi anaonyesha tu mapambo ni mapambo tu I: Kuna mitemba mingine udongo wake unaonekana ni mwekundu na mwingine unaonekana mweusi? R: Siwanatia rangi I: Kwahiyo ulikuwa unatiwa rangi? R: Eeeeh I: Ni rangi gani walikuwa wanapaka hapo ambayo ilikuwa inaweza ikachomwa na moto na isiharibike? I: Hiyo rangi nyeusi walikuwa wakiitengeneza kwa kitu gani? R: Hiyo hiyo udongo I: Na ‘Mtemba’ wa design kama hii ulikuwa ukitumiwa na watu gani hasa maana kulikuwa kuna matabaka kwenye jamii kwamba wazee labda wa hadhi fulani labda wametoka kwenye koo za kifalume? R: Hapana I: Mtu yoyote alikuwa akitumia? R: Ndiyo alikua akitumia I: ‘Kiko’ au ‘Mtemba’ R: ‘Mtemba’ I: Na ‘Mtemba’ huo kwa sasa hivi unaweza ukauzwa kwa shilingi ngapi ukiletwa sokoni? R: Ni kama hiyo shilingi elfu mbili

chanzo: Amani-Stade Project / Mlalo Field Research 2023, Interview No. 02
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
  • National Institute for Medical Research (NIMR) (Mteja)
  • unknown actor (wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali
  • Mlalo
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museen Stade, r 2018 / 18566jifunze zaidi
Mwandishi: Karl Braun, Nukuu/Angalizo: Museum der Kulturen Basel, VI 56197, 46 (118)jifunze zaidi
Asili ya data ya kitu
Museen Stade
Leseni
Creative Commons Namensnennung, nicht kommerziell, keine Bearbeitung 4.0jifunze zaidi
Imepitishwa katika lango imewashwa
2025-12-04T15:35:58+01:00

Rekodi zetu za takwimu zinafanyiwa maboresho kila mara. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali au maoni au ikiwa unahitaji taarifa zaidi au nyingine zinazohusu mali hii. Taarifa juu ya ulinzi wa takwimu.
Rudi kwenye utafutaji