Wakati
2023-06-19
Maelezo
I: hata ukiwa unaenda kwa mzee [anonymous] unaziona nyingi sana upande huu wa kushoto...sawa sasa tumemaliza picha zetu za postcard na sasa tunaenda kwenye picha za vifaa, na mkononi mwangu hapa nina picha ya kifaa ambayo imsajiliwa kwa namba 2018_18443_1, hebu angalia unweza ukafahamu ni kitu gani hiki
R: hiki kifaa kinaonekana ni ring ya shaba ambayo tamaduni za ujana wa zamani watu walikuw wanavaa ring mkononi, kwa hiyo hii ni ring ya shaba ambayo ilikuwa inavaliwa
I: unaweza ukatuambia kama ilikuwa na jina maalum kulingana na makabila ambao uliona wakitumia ring hiyo
R: ndio, wenyewe walikuwa wanaita 'nanga'
I: hicho ni kiliugha gani
R: hiyo ni lugha ya kiswhili, kwamba hii walikuwa wanaona vijana kwamba akivaa hii akikorofishana na mtu akimpiga roba ya kabari, kw hiyo hii inachukua kama sehemu ya silaha inamsaidia kumbana vizuri huyo mtu
I: na kwa makabila ambyo unayafahamu yalikuwa yakitumia hiyo unaweza ukatutajia makabila matatu hivi
R: hii ilikuwa ni kama culture fulani inaenea kwa makabila yote kwa hiyo wasambaa wa huku walikuwa wanatumia, wanyamwezi walikuwa wanatumia na makabila na wasukuma, mpaka leo hii ukiwaangalia wasukuma bado wanavaa, wajaluo bado wanavaa, ukieda sehemu za huko bara utaona watu wengi bado wanava hizo ring mikononi
I: labda kw wasambaa ilikuwa inajulikana kwa hilo la 'nanga'
R: ee walikuwa wanajua, hilo jina nililokutajia ni la wasambaa wanaita 'nangaa'
I: maana yake
R: maana yake hii shaba ndio jina lake kisambaa
I: na ikishatengenezwa bangili sasa nanga inaitwaje
R: bado wanaita vile vile
I: hivyo hivyo nanga
R: ee
I: na kitu hiki kilikuwa kinapatikana mikoa gani hasa
R: hizi shaba hakuna mtu anaitafuta hii shaba isipokuwa vifaa kama vile nyaya za zamani zilizokuwa zikitengenezwa zlikuwa zinatengenezwa kwa shaba, hata nyaya za umeme mabakuli, sufuria zilitengenezwa kwa shaba, kwa hiyo kulikuwa na mafundi mchungo ambao wanagonga na kutengeneza kubadilisha uelekeo wa kifaa kilichokuja na kutengeneza kitu kingine
R: kwa hiyo nanga ilikuwa inatumika mikoa gani hasa
R: tusemem ni tanzania nzima, kwa sababu zamani kulikuwa na masufuria ya shaba, mabirika ya shaba na vitu vingi vya shaba, kwa hiyo kikishachakaa jamaa wanavigongwa wanatengeneza kitu kingine kama kile cha kuvaa
I: na kipndi cha ukoloni sufuria ya shaba ilikuwepo
R: ndio yalikuwepo, na ndio hao walieneza sana kwa sababu nadhani aluminium ilikuwa haifahamiki zaidi ndio maana walikuwa wanatumia shaba, kwa kuwa wenyeji wlikuwa wanatumia sana vyungu vya kienyeji, na hii shaba uaniona jinsi ilivyokuwa imepungua, zamani haya masufuria ya shaba haya ukipika mboga huwezi kuweka limau, ukiweka limau inakuwa chungu, shaba huwezi ukaweka limau, ukiweka limaua inakuwa chungu kabisa kama shubili
I: kwa nini
R: nafikiria kuna asidi fulani ambayo haielewani na ile shaba, na ndio maana hii inachakaa hivi, inamaana labda katika kijipaka mafuta au nini ndio maana ikabadilika badilika hivi
I: na waliokuwa wakivaa nanga kwa kipindi hicho walikuwa ni watu jinsia gani
R: ni wanaume
I: kuanzia umri gani
R: ni vijana tu, anavaa bangili moja tu
I: nadhani nanga kwa sasa bado inaendele kutumika au itafika wakati itakuwa haina thamani tena kwa vijana
R: kutokana na miaka jinsi ilivyokwenda watu wamebadilisha kwa sababu siku hizi kuna tamaduni za aina nyingi, ukifika sehemu za bara utakuta bado kuna watu wanavaa, hata humu bado kuna wachache ambao wanavaajapokwa sio nene kama hili, maana hili ni zito sio nene kama hili lakini wanavaa, kwa mfano mifano ya hiyo nanga bado upo ukifika kwa wamasai utakuta wao bado wnavaa bangili za shaba japokuwa zimebadilishwa dizaini sio kama hivi bado wanavaa, wasukuma bado wanavaa na wasukuma wameboresha zaidi sasa hivi wanazaa hata mipira fulani mieupe wanakatakata waniunga wanavaa, kwa maana hiyo hii bado inatumika
I: na ili mtu atumie nanga kuna kitu kingine ambacho walikuwa wanapaswa kuwa nacho sambamba, yani anakivaa pamoja na nanga
R: hapana, ile ni kwa ajili ya ujana ujana tu, mtu anaona kwamba nikivaa hiki nitakuwa smart zaidi nitapendwa basi...
wote: wanacheka
I: kupendwa na akina nani
R: yani badala ya kuvaa saa anapata kitu ambacho kinamshughulisha mkononi
I: na ilikuwa ina umuhimu gani katika tamaduni za watu uliowataja
R: ni mapambo tu, hakuna kitu kingine zaidi ya mapambo
I: ni watu wa jinsia gani waliokuwa wakitengeneza nanga kipindi hicho
R: watu waliokuwa waktengeneza ni mafundi mchundo, nikisema mafundi mchundo sijui kiswahili kimeelekea maana mimi ni mswahili zaidi, ni hawa mafundi ambao wanatengeneza hata masufuria, ndoo na nini, ndio hao zamani walikuwa wataalam wakutengeneza vitu kama hivyo, ukikiangalia vizuri kwa mtu akikiangalia ambye hakuona hivyo vitu vya zamani hawezi kugundua kwamba hiki ni nini, lakini kwa mimi kwa sababu niliona napata idea hiyo
I: walikuwa ni wakike au wa kiume waliokuwa wakitengeneza
R: wakiume, nafikiria hata mimi ndani nikitafuta vizuri nitakuta ya babu yangu ninayo
I: sasa babu kama utaweza kuiona itakuwa ni vizuri zaidi
R: ngoja nitaitafuta
I: ni wa umri gani hasa walikuwa wakitengeneza
R: hii haina umri, zamani vijana walisifika kwa uhodari wa kutengeneza zana mbalimbali kwa maana hiyo kila aliyejifunza aliweza kutengeneza
I: na kwa sasa katika maeneo tunayoishi hapa amani kuna mtu anayetengeneza vitu kama hivyo
R: hapana, kwa sababu sasa ukikuta watu wamevaa ring kama hizi sio ring tena ni vitu vimedariziwa kwa ushanga aidha chata ya simba au ya yanga ndio watu wanavaa
I: sawa, hapo ndio tumeweza kutambua kwamba ni shaba ndio ilikuwa inatumika kutengeneza hiyo, kwa ya kadiri miaka inavyozidi kwenda na kubadilika, nyenzo zilizokuwa znatumika kutengenezea nanga zilikuwa zikibadilika pia au ziliendelea kuwa shaba mpaka leo
R: nyenzo zimebadilika baada ya kutokea vitu kama vile almunium, lakini hii ya babu yang ninayoizungumzia bado ni ya shaba hivi hivi, ina uhalisia huu huu lakini itabidi niitafute maana ina miaka mingi sana
I: na ukingalia nanga hiyo na uhodari ilivyonakshiwa, ikiletwa katika sokola leo inaweza ikauzwa shilingi ngapi
R: sidhani kwa sababu anayenunua lazima ajue kwamba hiki kitu ninakinunua kwa faida fulani na thamani fulani, ila sasa hivi ukimpelekea mtu anaweza akatengeneza heleni badala ya kutengeneza nanga tena kwa sababu nanga tena hazivaliwi, inaonekana shaba iliyokuwa inatumika hapo zamani ni ile shaba nzuri
I: kwa mantiki hiyo shaba hiyo tuchukulie tunauza material, kwa shaba hiyo inaweza ikauzwa shilingi ngapi
R: itaweza ikawa na thamani kama ya shilingi hela za kitanzania kama labda kwenye elfu 50
I: kwa sababu gani umetoa thamani hiyo
R: hii ni nzito, ni shaba nzito nene, kwa maana hiyo kama ukikata vipande na kudizaini vitu vingine vidogo vidogo inatoa vitu vingi sana kama vile heleni, mikufu inaweza ikatoa vitu vingi sana
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 25
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali