Wakati
2023-06-15
Maelezo
I: sawa, tunaenda kwenye picha nyingine, hapa nina picha ambayo imesajiliwa kwa namba 2018_18384, hebu angalia, unatambua hicho ni kitu gani
R: haya ni mavavi ya wajumbe, yaani ni kama hivi jumbe joho ambapo sasa hivi wanasema ni madiwani sijui waheshimiwa wabunge, lakini sasa hivi haya mavazi ukiyaona ni ya watu wakubwa sana...
I: yalikuwa yanaitwaje kwa kipindi hicho mavazi kama haya
R: kwa kipindi hicho walikuwa wanaita ‘vikoi’, yani baada ya kuvaa kanzu unavaa na kikoi, lakini kikoi sio mtu wa hovyo hovyo ambaye alikuwa anavaa, waliokuwa wanavaa ni watu ambao ni maarufu kama 'jumbe salimu, jumbe kika, jumbe joho.
I: hao majumbe walikuwa ni wakabila gani
R: sana sana ni wa kilindi, hao wengine ni wadoe tu, lakini ni wakilindi ambao wanamaliza kesi, akikuambia unakwenda kufungwa unaenda kufungwa ndio walikuwa wanavaa mavazi hayo, na mkimuona kama jumbe joho, tena akiingia kwenye mji wenu mnatafuta hata mbuzi ili mchinjie kwamba kuna mambo ambayo mnayaweka sawa
I: na walikuwa wanayapata wapi mavazi haya
R: mavazi haya kwa kweli kuna DC au PC, yani kuna watu ambao wako kwenye serikali ndio wanajua kwamba tukija hapa tumkute joho ndio wanatoa hili vazi, ambapo hili vazi nalo sijui wanaliotoela wapi, aitha wamelinunua huko wanaleta, na hao wanaleta kwa mtu maarufu kwenye kile kijiji, unaona mpaka sasa hivi kuna jumbe kama akina jumbe salimu hapa na wengineo akina jumbe mdoe, wazungu wametusogeza ndio maana sasa hivi hatuna maeneo, sasa kwa vile ameshavalishwa hili anasema tunapanda chai na sisi tunakubali tunalipwa hela na tunaachia mashamba yetu...
I: na wao ndio walikuwa wanamamlaka kwa wananchi wao?
R: ndio akisema hasa kwa kilindi, na akivaa vazi hili sio kwamba ni siri, akikuambia huyu mke ni mamurugu anamchukua, muulize hata mzee chei, anakuambia ni mamurugu kwamba yule mke wako sio wa kwako tena anamchukua akivaa vazi hilo,
I: anacheka...
R: sio kwamba ni siri, akishavaa vazi lile jua ni bwana mkubwa hata akiingia nyumbani mwako wewe uko radhi uangalie kando lakini akikuambia mke wako ni mamurugu kweli anamchukua, na ndio maana utakuta makabila wengi sasa hivi.tume... sijui ni nini, hata mzee chei hili analijua hili vazi na anajua baba zao walivyofanya, maana utakuta mzee chai kwenye nyumba yao sio ajabu walikuwa wanawake wengine walikuwa ni wanawake wa watu wameletwa mle, ndio unakuta kuna makabile mengi, wengine ni weupe, wengine ni weusi, lakini ni majumbe ndio wanaovaa mavazi haya
I: walikuwa wanavaa kipindi gani mavazi hayo
R: haswa kipindi cha siku za kesi au siku za sherehe, au siku kama kuna ngoma hizi ambazo wenyewe wanakwenda kutambikia au kuna mkutano fulani sio wa kijiji, ni mkutano ambao labda labda watoto wanataka waende wakathiriwe au wakafanyiwejando, basi wanavaa hili na hao wenyewe ndio wanakaa kwenye vile viti vya kifalme wanaamua kitu kama hicho, lakini haya mavazi mimi nayakumbuka kabisa mzee jumbe joho au kama kuna mwenzake amefariki anataka arithi basi anavaa hili na kanzu yake na fimbo yake, anakua na fimbo na kanzu na hii scarf, basi akija pale akishachukua bunduki yake... sio hizi bunduki za sasa hivi , kuna zile bunduki za kuchochea hivi, magobole yale, akipiga hapo basi unajua huyo atarithi huyo mke, yuko radhi ajaze hata wanawke sita wenzao kama wamefariki ambapo sasa hivi watu hawataki kurithiana kwa ajili ya maradhi, kweli sio kwamba ni siri haya mavazi yananikmbusha mbali kwamba ni ya majumbe
I: majumbe walikuwa wanaanzi umri gani na ni wa kike au wa kiume
R: ni wa kiume haswa
I: kuanzia umri gani
R: mtu akishafikisha kama miaka 40 au 30, akishaozeshwa basi, 40, 50 na kuendelea, akiozeshwa basi na huwezi ukaoa kama sasa hivi, ukitaka kuoa wanakuambia uende nyumba ya mohamedi ukaoe mtoto wake, sio kama sasa hivi tu mnakutana mitaani, ni ile nyumba babayake ni mzuri na mama yake ni mzuri na huo ukoo utakuwa ni mzuri
I: sawa, sawa, vikoi kama hivyo vinatumika hivi sasa?
R: ah, sasa hivi si watakucheka
wote: wanacheka
I: unadhani kwa nini watakucheka sasa hivi ukiva kikoi kama hicho
R: mambo ya kale hayo, unaona hata suruali zetu sasa hivi, hata sisi wazee pia tunajitahidi tuvae suruali za kisasa, sijui ni kwa nini na watu tunaenda na wakati, kisha mavazi kama haya yalikuwa yanasinga na ni mavazi yenye heshima lakini watu hawayapendi wanakuambia umepitwa na wakati, zamani ukivaa lile lo, hata akina mama huko wenyewe wanajua anapita jumbe sio ajabu atanipenda mimi, na watu wa zamani walipenda sana wanawake weupe, sijui kwanini, kwamba ukioa mke mweupe ujue atakwenda na majumbe tu
wote: wanacheka...
R: sio siri, ndio maana wakilindi wengi... usioe mke mweupe kilindi atamchukua atamchukua tu, wajumbe wanaovaa haya watambeba tu, sijui kwa nini wenyewe.
I: na wao vazi hilo lilikuwa lina umuhimu gani kwao
R: halina umuhimu bali tu ni kitu ambacho unajua kwamba huyu ni fulani, kama hivi wachezaji wa mpira kuwatambulisha ni timu gani, hata akiingia kijiji hiki hata humfahamu lazima tutaamka tukampokee jumbe na wote hata kofia tunaona wote, tena kwa kumuongoza vizuri, na awe anaenda kwa jumbe salimu, au anaenda kwa jumbe kika au kwa jumbe nani, anauliza jumbe fulani yuko wapi, mnamwambia yuko hapo basi mnampeleka, tena kwa mwend wa pole pole, si ana lile vazi...
wote: wanacheka...
I: na labda niulize, jumbe yule anaweza akaja ameoa labda ana miaka 40 lakini ndani ya ile jamii kuna watu wa miaka 60,70 ,80, akiwa amevaa hilo vazi hata hao wazee pia wanamheshimu?
R: wanaamka, lazima wataamka, wewe labda huna asili ya ukilindi au huna asili ya kuvaa haya, sijui unatafuta kwenda kupigwa kigongo uende ukafie huko halafu watu kaburi yako watu wasiione, lazimu wamuheshimu hata kama unamiaka 50, 60, 70, lazima umuhesimu jumbe, yani kama mambo ya kifalme, haya mavazi mimi ninayakumbuka sana, na labda wengine walilirithi lakini baadaye sijui mavazi yalikwenda wapi, ninakumbuka hapa nyumbani kulikuwa na mzee mmoja baba yake huyu mkande atakuambia hili vazi, ilikuwa siku za iddi wakishamaliza sijui siku 30, akilivaa hili halafu na fimbo yake na scarf yake basi wanacheza, yani kama umwinyi mwinyi...
I: umesema kulikuwa na kanzu, fimbo, scarf na kikoi, ni kitu gani kingine walikuwa wanavaa pamoja na vazi hili
R: kilemba
I: cha rangi gani
R: rangi aina yoyote lakini sana sana kuna vilemba vile vya rangi nyekundu, au nyekundu, vinafanana na hivi hivi, kulikuwa kuna mavazi wajerumani sijui waliwaletea kutoka ujerumani, utafikiri ni kama wale maaskofu, ni mavazi kwa kweli kwanza huwezi ukaligusa na wala halifuliwi na mtu yoyote...
I: anacheka...
R: labda mke wake wa kwanza ndio anaruhusiwa kuligusa, na hapo lipo kwenye sanduku za mbao likitolewa hilo kuna manukato fulani ya dawa za sanduku, akitoka jumbe hapo anaangaliwa maana tunamgojea jumbe, hayo maelezo ninayoeleza ni vitu ambavyo nimeviona kwa macho yangu nikiwa sijui niko darasa la 5 la 6, nawaona nikasema hawa watu... baba alikuwa ni muislamu lakini baada ya kusoma misheni ikabidi aingie ukristo, na mimi nilikuwa naona nauliza haya mavazi wanayatoa wapi, mimi mwenyewe tu nina kaptula huko ndani sina chochote, lakin ile kaptula na shuka ile...
I: labda unaweza ukatuambia kwa sababu mavazi hayo umeyaona, ukiangalia yalikuwa yanatengenezwa kwa kutumia kitu gani
R: mh, hapo sijui labda huko ujerumani kwao, lakini sana sana ni pamba ambalo tulikuwa tunalilima sisi wenyewe, pamba ambalo tunapeleka nje, pamba katani, ni vitu vingi na vitu vingi sisi tulikuwa hatujui thamani yake, tunalima tu lakini wenzetu wakija wanachukua, sasa hivi hata huyo jumbe aje avae hivi utasikia 'huyu mzee ana nini, anaenda wapi sasa hivi', lakini mzee utampata nani sasa hivi, lakini mzee utampata nani sasa hivi, labda kama mzee chei tu ndio kama amebakia sasa hivi, lakini wazee wengi jumbe salimu amefariki,na kuna wazee wengi sana ambao walikuwa wanavaa hayo mavazi ambao ndio wajumbe, sisi wengine tulikuwa tunaitwa wadoe, yani wdoe ni watu wanaosikiliza kesi tu, lakini mwenye vazi hili ndio amekaa kwenye kile kiti kama pale Chemka , mzee jumbe joho au jumbe mkande pale Chemka, yani wana ngazi zao, ukitoka huku Kazita kuna jumbe, lakini kuna jumbe wao mkubwa kama yule mzee wa hapa Derema hapa Kwekuyu, jumbe joho yule naye alikuwa ni mtu mmoja maarufu sana, hata amani kule akiingia wazungu pia walikuwa wanamjua kwamba ni jumbe joho, hata akitembea mwendo wake anatembea pole pole, haya mavazi kwa kweli yana sifa zake zamani kwa kweli, sasa hivi hamna
I: labda tulilete vazi hili kwa hali yetu ya sasa, likikutwa sokoni kwa anayejua thamani yake anaweza akalinunua shilingi ngapi ukikadiria kwa sasa
R: ah, watakuambia labda elfu 10 au elfu 20 au hata 50 mtu anachukua lakini... ni mavazi yenye thamani kubwa sana lakini sasa hivi mtu tena hata anaweza hata bei asiliulize asilione umuhimu wake maana hajui umuhimu, inatakiwa ukinunua kitu labda una umuhimu nacho lakini kitu ambacho huna umuhimu anaweza akakuambia nikupe shilingi elfu 5 nimpelekee babu yangu, ambapo kwamba zamani thamani yake ilikuwa ni kubwa sana.
I: na kwa maelezo uliyotuambia kwa sasa ingeuzwa ghali sana kutokana na hadhi ya hilo vazi jinsi lilivyokuwa likitumika
R: ingekuwa hata laki tatu nne mtu anannua kwa sasa hivi , halafu kuna haya mashada ambayo yako humu kwenye kola, hivi vitu ambavyo ni vya thamani sana; kwanza hata kumsogela huyo jumbe akiwa kavaa hivyo sio rahisi kwa kweli, kwa kweli sio siri wenzetu wa zamani wamefaidi sana na heshima zao wamezipata, na sijui kama vitarudia tena hivi, sasa hivi tu mtu ni mwenyekiti lakini anaambiwa wazee benchi lote limeoza hilo, zamani useme hivyo si una...
Wote: wanacheka
R: sio siri, sasa hivi umekaa pale wewe ni mwenyekiti halafu ah, benchi lote limeoza hili...
I: unataka kupigwa rungu...
R: kwanza utathubutu hata kunyosha kidole... wewe unaangalia chini tu hivi, sivyo huendi kuzikwa, ndio maana utakuta kuna sehemu nyingine zenye mapango kule, utakuta mafuvu; utasikia huyo nenda ukamgone rungu, hata ukizaa mapacha wanaua mmoja abaki mmoja au wote wanauwawa
I: kwa nini
R: walikuwa wanasema sio vizuri watoto wawili, yaani wanasema sijui ni mbegu mbaya yaani hawatasikia, lakini sasa hivi kumbe mapacha ndio ambao wana akili, lakini zamani ukizaa mapacha au zeruzeru wanawaua
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 21
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali