Wakati
2023-06-15
Maelezo
I: sawa, tuna picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18320_001 hebu angalia, unaweza ukatmbua ni kitu gani hiki
R: hii ni fimbo tu ambayo wale wanaovaa majoho ndio wanashika hizi fimbo
I: hizo fimbo zilikuwa zinaitwaje kisambaa
R: hapa mbele wanaweza wakachonga kama wanavyofanya wamasai, wanachonga kama sura ya mtu au mnyama wa aina yoyote, lakini sana sana kuna miti ile wanaita mpingo ambao ni mgumu sana ambao wanachonga, ni fimbo ambayo wale wanaovaa majoho wanapenda sana kisha hizi wale wa kilindi, huoni kama hii hapa sio ndege huyu ambaye amechorwa...
I: ni kama sungura hivi
R: ni kama sungura na masikio, sasa hata wewe unayempokea...
I: ilikuwa ina jina maalum fimbo hiyo ikitumiwa na hao watawala
R: wanasema fimbo ya mfalme au ya jumbe, na hazishikwi na watu, zinashikwa na watu maarufu
I: kama hao wa kilindi...
R: wa kilindi haswa, wa kilindi wenzetu walichukua nafasi kubwa sana ambao hata sasa hivi kweli sio siri hawako ...sio wale wa kilindi, walikuwa ni a kipindi hicho, sasa hivi ukiitwa mkilindi unasikia 'ah achana na mkilindi wamekuwa hapo zamani', manake zamani anaweza akakuambia huyu mke ninamchukua mimi, tena sio kwamba anamchukua, akishamuangalia anawaambia 'nendeni kwa bwana hiza, mwambieni yule awe wamurugu' akishaitwa jina la 'wamurugu', kweli akija anachukuliwa anakuja kwenye nyumba, au kama sivyo anawambia kama hamuamini nendeni na hii fimbo, akija anaambiwa hii fimbo ni ya jumbe...
I: fimbo kama hii
R: ee, kama hii, hii fimbo ni ya jumbe, na hakuna mtu mwingine ambaye anaweza akashika hii fimbo, anayeshika hii ni jumbe, sasa anayetakiwa ni mtoto wako eti aende kwa jumbe
I: kwa hiyo fimbo ilikuwa inatumika kama sehemu ya kukaba...
R: sehemu kama ya kukomoa komoa watu ambao hawana nafasi nzuri, yani walikuwa na vitu vyao, kwa kweli ukoloni na sasa hivi... tuwashukuru wazungu wametulete... na pia tumshukuru na nyerere, lakini ingekuwa bado sasa hivi tuko kwenye mambo ya kutawaliwa, lakini sasa hivi huoni mpaka sasa hivi hata nyinyi pia mmepata elimu mnakumbuka mambo zamani hvi, kwa sababu hata mimi mwenyewe nisingekumbuka kabisa, yani sio rahisi, lakini serikali sasa hivi inatumia utafiti huu, ujue kwamba ni jambo la kukumbusha, mzee chei pale pia si unaona kuna sahani zile pale zina mtu anachota maji na sahani ni ya dongo.
I; fimbo kama hizi zilikuwa zinapatikana zaidi katika mikoa gani hasa
R: mkoa wa tanga, handeni, hasa hasa mkoa wa tangau masaini huko, singida huko, kama hivyo akina chifu mkwawa, iringa kule, iringa bado mpaka sasa hivi mambo ya mila wanayo, bado iringa wana mambo ya mila, yani iringa na huku kwa chifu mkwawa na huku tanga kwa wakilindi, wakilindi walitawala sana, wabondei walikuwa naona safi
I: kwa hiyo sasa hivi haitumiki kabisa hii fimbo
R: sasa hivi kwamba kuipata, utaipata wapi, na watu wanajtahidi wanatafuta tafuta fimbo kama hizi, sasa miti iko wapi ni mbuga tupu, ilikuwa zamani tembo na chui zinapita humu, mbuzi wanakimbizwa na chui, sasa hivi hata sehemu za kuchungia hamna, ni mashamba tu
I: kwa hiyo hata kutengenezwa sasa hivi hazitengenezwi tena
R: kwanza ukishika fimbo wanakuambia ‘huyu naye anajiingiza kwenye uzee’
wote: wanacheka
R: fimbo tu nasema inisaidie kama ile ya mzee chei pale, anakuambia mbona umekuwa mzee mara hii, kwa kweli mimi nimeshukuru kwa kunikumbusha mambo ya zamani, yani nashukuru sana
I: hebu niambie, fimbo hizo walikuwa wanatengeneza watu wa jinsia gani
R: kuna watu wenye fani zao kama hizi, unaweza ukaambiwa tengeneza fimbo hii kama watumwa watumwa hivi, unaelekezwa, fanya hiki fanya hiki na wale machifu, tengeneza hivi na hivi, chonga hivi, kuna visu vile vilikuwa vinaitwa okapi, sasa vile vinachonga, vile visu yani ni vikali mno, basi ukija unaambiwa tengeneza hivi, chonga hivi , fanya hivi...
I: na hii picha inaonekana inang'aa, inawaka vizuri, walikuwa wakipaka nini mpaka ionekane kiasi hiki
R: saa nyingine wanaweza wakapaka mafuta ya ng'ombe, ni sawa sawa na mwanamke akizaa inachinjiwa mbuzi anapakwa yale mafuta, mwanamke akitoka hata kama ni siku mbili tatu unamkuta ameng'aa kwa ajili ya yale mafuta wanayompaka, halafu na mila mara siku ya kwanza siku ya pili mwanamke unamkuta sokoni...
wote: wanacheka
I: mzee hiza, fimbo hiyo kwa mazingira ya sasa hivi, kwa wewe unayeijua umuhimu wake unaweza ukainunua shilingi ngapi sokoni
R: hii ninaweza nikainunua kwa shilingi 20, 30, nainunua ili niwekee watoto kumbukumbu, kama sasa hivi nimeona vitu vya mzee chei pale kamera ile, kuna sumaku, ile kamer ina sumaku, tena yule mzee kuna vitu vingi watoto wake wamebeba beba wale wanaojua, kwa hii fimbo nikiipata ingawa hata siku moja ninaweza nikapita nayo ingaw watanicheka
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 21
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali