Wakati
2023-06-10
Maelezo
I: Sawa nina picha nyingine hapa imesajiliwa kwa namba 2018_18279_001 hebu angalia unaweza ukatambua ni kitu gani hichi mama?
R: Mkoba
I: Ni nini?
R: Mkoba
I: Mkoba ni kilugha gani hicho?
R: La kisasa lakini zamani tunaita mfuko
I: Mfuko kwanini mlikuwa mnaita mfuko?
R: Hawa wenzetu wanavyoita mkoba hivyohivyo ee
I: Kwahiyo mfuko na mkoba ni kitu hichohicho?
R: Kimoja
I: Ni kabila gani wanaita mkoba?
R: Kisambaa
I: Kisambaa wanaita mfuko?
R: Eeeeh
I: Ni ulikuwa unapatikana zaidi mikoa gani mifuko kama hii?
R: Tulikua tunanunua sehemu za Muheza, Tanga
I: Muheza na Tanga?
R: Eeeeh
I: Ulikuwa unatumikaje huo mfuko?
R: Ni mkoba tu wa kutembelea kwenda sokoni basi
I: Unatembelea kwenda sokoni, sokoni unaenda kufanyia nini?
R: Kuwekea vitu
I: Vitu kama nini?
R: Mboga, kuna nazi kuna vitu vyote vinavyotumika ndani
I: Mkoba kama huo unaweza ukatumikaje kwa namna nyingine ukiachia kwendea sokoni?
R: Huu
I: Eeee
R: Kwa namna nyingine sijui mimi najua kuwekea vitu tu
I: Kuwekea vitu tu?
R: Eeeeh kuna mikoba ya uchawi sasa hiii sisi tunatumia kwa kuwekea vitu
I: Lakini wengene wanatumia kufanyia nini?
R: Kwa uchawi
I: Uchawi?
R: Eeh anaweka vitu vyake humo ndiyo unakuwa ni mfuko sasa
I: Mfuko?
R: Eeeeh
I: Hebu tuweke tofauti ukiwa ni mkoba ni kwa matumizi ya nini?
R: Ndani
I: Ukiwa ni mfuko?
R: Ni hivyo hivyo matumizi ya ndani
I: Ya ndani?
R: Eeeh
I: Umesema mfuko unawekewa uchawi?
R: Eeeeh
I: Na mfuko nao unawekwa uchawi?
R: Eeeeh lakini zamani walikuwa wanatumia sana vikoba hivi eeh kuwekea vitu vyao vya kiganga
I: Vya uganga?
R: Eeeeh
I: Ahaaah
R: Lakini sisi tunatumia kuendea sokoni na kuwekea vitu vyako basi
I: Kwenye vya uganga walikuwa wanatia nini sana humo
R: Humo ndani
I: Eeeeeh
R: Kuna yale mapembe uliyoyaona sisi situmeuguliwa maana kwa kuuguliwa tumepitia kwa kweli lakini saivi sasa hata
I: Kwahiyo ulikuwa unatumika kwa matumizi mawali
R: Eeeeh
I: Kununulia vitu masokoni?
R: Na wengine wanawekea uganga wao wasili
I: Uganga wao?
R: Eeeeh
I: Kwahiyo wanaowekea uganga ni wale wanaotibu kwa kutumia waganga wa jadi?
R: Eeeeh waganga wa jadi
I: Inakuwa kama nini hasa?
R: Wanahifadhia vitu vyao
I: Na jinsia gani walikua wanatumia Zaidi mikoba hii?
R: Wakike
I: Wa kike?
R: Eeeeh
I: Wa kike wa umri gani?
R: Wa kina mama wazee tu
I: Wazee?
R: Ndiyo wanaofanya kazi hii eeh
I: Eeeeh
I: Na wanaounda watu gani?
R: Watu wa bara?
I: Makabila gani hasa?
R: Hao hao niliokutajia
I: Nikumbushe umenitajia makabila mengi kidogo nimeshayasahau?
R: Wafipa wamambwe, wanyakyusa, na wanyamwanga
I: Wafipa ni sumbawanga, na wanyakyusa?
R: Ni huko wanaita sikujui
I: Mbeya ni mbeya au Iringa wanyakyusa Mbeya, wanyamwanga
R: Na wamambwe
I: Wamambwe ndiyo walikuwa wakitumia zaidi hiyo
R: Eeeeh
I: Wao walikua wanatumia zaidi kwa ajili gani?
R: Kama hapo Monga walikuwa wanauza
I: Kwenye masoko?
R: Eeeeh
I: Soko la siku gani walikua wanauza Monga?
R: Jumamosi na jumatano
I: Jumamosi na jumatano?
R: Eeeh
I: Waneleta mpaka leo?
R: Saivi ahhh ni muda taingia sijafikisha watoto wangu wawili
I: Lakini soko bado lipo?
R: Soko lipo si hilo banda hapo lile banda kubwa pale
I: Ila mikoba kama hiyo hailetwi?
R: Hamna saivi
I: Aaaaah
R: Saivi hata mkeka hauukuti
I: Kwahiyo kwa mawazo yako unadhani haitumiki tena au?
R: Haitumiki imekufa
I: Kwahiyo hata watu wa uganga hawaitumii pia?
R: Sijui sasa kwa waganga ee maana saivi siwanasema wanaenda na mtandao
I: Hahahahah hata kwenye uganga napo wanatumia mtandao?
R: Mtandao eeh kwasababu kila kitu kinabadilika
I: Hahahaha
R: Maana akiuweka mkoba wake anajulikana anasafiri kumbe anaenda kutibu
I: Hahahahah ni mtandao siku hizi?
R: Eeeeh maana akiweka hivi atajulikana ni mganga hahahhahah
I: Hahaaha kwahiyo humo ndani walikuwa wanahifadhia mapembe ana kitu gani kingine walikuwa wanaweka humo?
R: Humo kuna vichupa, mapembe sisi tumeuguliwa kwahiyo vikitolewa unaona
I: kilikuwa na umuhimu gani mkoba huu ulikuwa na umuhimu gani kwa makabila uliyoyataja?
R: Wao ni kwendea sokoni kwa kweli
I: Sawasawa kwasasa havitengenezwi?
R: Sahivi hamna
I: Na waliokuwa wanatengeneza mikoba kama hiyo ni jinsia gani wa kike au wakiume?
R: Wa kike
I: Wa kike?
R: Eeeeh
I: Kwanini walikuwa wanatengeneza wa jinsia ya kike?
R: Wanatafuta hela
I: Wanatafuta hela?
R: Eeeh
I: Wakiume walikua hawatafuti hela?
R: Mwanaume ni pombe na yeye
I: Hahahaha kwahiyo akina mama ndiyo walikuwa wanatafuta hela kipindi hicho cha zamani ndiyo watafutaji?
R: Eeeeh
I: Wanaume wao kazi yao ni kunywa pombe tena kwenye pembe?
R: Eeeeh
I: Hahahahah sawasawa na unaweza ukatambua walikuwa wanatengeneza kwa kutumia vifaa gani?
R: Walikua wanatengeneza sindano lakini siyo sindano hizi za kushonea kuna sinda no zenyewe wanazotumia eeh
I: Na haya material gani wametumia hapa?
R: Wamesuka hapa wamezungusha siyo ukindu lakini ni huu niliokuambia wanashona virago
I: Virago?
R: Eeeeh madude yako humo mtoni
I: Wanaitaje?
R: Sijui Jina Lake
I: Sawasawa na miaka yote mpaka mara ya mwisho unaacha kuona vitu vilivokua vinatumika vilikuwa ni hivo hivo?
R: Eeeeh
I: Haujawahi kuja wa tofauti?
R: Hapana
I: Maana siku hizi kuna plastiki
R: Eeeeh saivi hamna
I: Mkoba kama huo ukiukuta sokoni kwa sasa hivi na wewe unaujua vizuri unaweza ukaununua kwa shilingi ngapi?
R: Saivi wanakuuzia wanakwambia elfu tano zamani tulikuwa ni elfu moja, au elfu tatu ndiyo mwisho eeh
I: Kwahiyo saivi umepanda bei?
R: Eeeh utaambiwa elfu tano
I: Kwanini bei inakuwa imepanda saivi?
R: Si mtandao
I: Hhahahaha mtandao ndiyo umepandisha bei?
R: Eeeh watu wanaenda na mtandao
I: Mtandao?
R: Eeeeh
I: Sawa basi mama sisi tuchukue muda huu kukushukuru kwa ushiriki wako umetusaidia kweli tumepata taarifa ya baadhi ya picha zetu hapa umechangia kwa kiasi kikubwa sana
R: Au siyo
I: Eeeee asante sana kwa ushiriki wako tukikugongea tena wakati mwingine utupokee kwa mikono miwili
R: Si ndiyo sawa
I: Hahahahah
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali